Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Maandamano kuungano mkono COP21 kufanyika maeneo mbali mbali duniani

Maandamano kuungano mkono COP21 kufanyika maeneo mbali mbali duniani

Siku kumi kabla ya kuanza kwa mkutano wa 21 wa nchi wanachama wa mkataba wa kimataifa wa mabadiliko ya tabianchi, COP21 huko Paris, Ufaransa, Mwakilishi wa kamtibu Mkuu wa umoja huo kuhusu mabadiliko ya tabianchi Janos Pasztor amezungumza na waandishi wa habari kuhusu maandalizi ya shughuli hiyo.

Mathalani amesema kuna masuala ya msingi ambayo yameanza kuangaziwa nuru kufuatia mikutano ya ngazi ya mawaziri na kwamba mambo hayo yanayohitaji zaidi uamuzi wa kisiasa yatawekwa bayana baadaye.

Hatua nyingine inayotia moyo ni ongezeko la idadi ya nchi zilizowasilisha mipango ya utekelezaji ya kitaifa katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

(Sauti ya Janos)

“Hadi leo asubuhi, nchi 171 ambazo zinasababisha karibu asilimia 90 za gesi chafuzi, tayari zimewasilisha mipango yao ya kitaifa kuhusu mabadiliko ya tabianchi na malengo. Iwapo hiyo itatekelezwa  vizuri, mipango hii ya kitaifa itashusha kiwango cha gesi chafuzi na hivyo kupunguza kiwango joto kinachotarajiwa kuongezeka kwa takribarni nyuzi joto Tatu katika kipimo cha selsiyasi ifikapo mwishoni mwa karne hii.

Kuhusu kufutwa kwa maandamano ya tarehe 29 mwezi huu mjini Paris kutokana na sababu za kiusalama, Bwana Pasztor amesema wanaheshimu uamuzi wa serikali ya Ufaransa na kwamba matumaini  yao ni..

(Sauti ya Janos)

“Kuwa viongozi na washawishi bado wataitikia sauti ya mashirika ya kiraia ambayo yatakusanyika na kuandamana kwenye miji yao mbali mbali duniani, sasa imefikia zaidi ya 2000 kuonyesha mshikamano wao na hatua kwa mabadiliko ya tabianchi mwishoni mwa wiki tarehe 29 Novemba kupitia maandamano ya amani.”

Mwakilishi huyo wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema zaidi ya viongozi 121 wameridhia kuhudhuria mkutano huo.