Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Sekta ya viwanda Afrika iajiri wanawake na vijana zaidi : Ban Ki-moon

Sekta ya viwanda Afrika iajiri wanawake na vijana zaidi : Ban Ki-moon

Leo ikiwa ni siku ya kukuza sekta ya viwanda barani Afrika, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema Umoja wa Mataifa uko tayari kusaidia biashara ndogo na za kati ili kuzalisha ajira zaidi na kutokomeza umaskini.

Kwenye ujumbe wake kwa siku hiyo, Bwana Ban amesema licha ya mafanikio makubwa ya kiuchumi barani Afrika kwa kipindi cha miaka kadhaa iliyopita, bado maendeleo hayo hayakuwa jumuishi hasa kwa vijana na wanawake.

Amesisitizia umuhimu wa kuwekeza katika mafunzo ya wanawake na vijana ili kukuza sekta binafsi ambayo huajiri asilimia 90 ya watu barani humo na hivyo kuhakikisha ukuaji wa uchumi unakuwa endelevu na jumuishi.

Bwana Ban amesema hiyo ndio njia ya pekee ya kutokomeza umaskini barani huo na kufikia maendeleo endelevu ifikapo mwaka 2030.