Skip to main content

Vijana wa Afrika wazingatia umuhimu wa kuimarisha hati miliki

Vijana wa Afrika wazingatia umuhimu wa kuimarisha hati miliki

Zaidi ya vijana 50 wavumbuzi, wabunifu na wajasiriamali kutoka Afrika, wamekutana mjini Dakar, nchini Senegal wiki hii, katika warsha ya kuzungumzia masuala ya hati miliki, uvumbuzi na ubunifu.

Warsha hiyo ya vijana kati ya umri wa miaka 18 na 35, iliandaliwa na Shirika la Kimataifa la Hati Miliki, WIPO, Japan, serikali ya Senegal na Muungano wa Afrika, ikifanyika kabla ya kongamano la ngazi ya juu la mawaziri kuhusu hati miliki kwa bara Afrika linapoinuka, kuanzia tarehe tatu hadi leo tahere tano Novemba.

Katika Makala ifuatayo, Joshua Mmali anakuletea baadhi ya sauti za vijana hao na mawazo yao.