Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Waethiopia warejea kwao kwa hiari kutoka Yemen na Djibouti: IOM

Waethiopia warejea kwao kwa hiari kutoka Yemen na Djibouti: IOM

Shirika la Kimataifa la Uhamiaji IOM limesaidia raia 54 wa Ethiopia waliokuwa wamekwama nchini Djibouti na Yemen kurudi makwao.

Kwenye taarifa iliyotolewa leo, IOM imesema kwamba miongoni mwao walikuwa vijana 22 wenye umri wa chini ya miaka 18 ambao hawakuwa na mzazi wa kuwasindikiza, akiwemo pia msichana wa miaka 12.

IOM imeeleza kuwa inaendelea na uchunuguzi kuhusu familia zao ili kuanza utaratibu wa kuwaunganisha upya, huku vijana wakihifadhiwa kwenye kituo cha IOM mjini Addis Abeba nchini Ethiopia.

Kupitia mradi wa IOM wa kusaidia watu kurejea makwao kwa hiari, mamia ya waethiopia waliokuwa wakiishi kwenye mazingira magumu Djibouti wamerudi makwao.

Mwezi Oktoba pekee, waethiopia 137 wamerejea nyumbani.