Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tusiwasahau masikini: Ban

Tusiwasahau masikini: Ban

Jamii ya kimataifa inahitaji kutupia macho jamii za pembezoni na waliotengwa na wanadamu amesema Katibu Mkuu Ban Ki-moon

Umoja wa Mataifa unakadiria kuwa kote duniani kiasi cha watu milioni  900 wanaishi katika ufukara.

Katika ujumbe wake wa kuadhimisha siku ya kimataifa ya kutokomeza umasikini Oktoba 17, Ban amesema dunia imepiga hatua kubwa katika kupunguza umasikini.

Mika 25 iliyopita, zaidi ya watu bilioni moja wameinuliwa kutoka katika kizingiti cha umasikini lakini wengine milioni 900 bado wako kwenye lindi la umasikini

Bwana Ban ameonya kuwa mabadiliko ya tabia nchi, machafuko na majanga mengine ni matishio katika kuendeleza juhudi za kutokomeza uamsikini

Ameongeza kuwa katika kupitisha ajenda mpya ya maendeleo endelevu mwezi Septemba , viongozi wa dunia wameweka ahadi ya muda ya kumaliza umasikini na aina zake, popote pale.