Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ajali kubwa zaidi ya wahamiaji , msaada wa haraka wahitajika: UNHCR

Ajali kubwa zaidi ya wahamiaji , msaada wa haraka wahitajika: UNHCR

Kamishna mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la wakimbizi António Guterres leo ameelezea kushtushwa na  ajali ya boti siku ya jumamosi  ilyowahusisha wahamiaji  katika bahari ya Mediterranean inayolezwa kuuwa idadi kubwa zaidi ambapo ni watu 50 tu kati ya 700 walionusurika.

Taarifa ya UNHCR imemnukuu Bwana Guterres akisema kuwa kufuatia janga hilo la kihistoria ametaka msada wa haraka wa uokozi kwa manusura wa ajali hiyo  huku pia akitaka pia suluhu la muda mrefu la uhamiaji wa kwenda barani Ulaya.

UNHCR imesema inafanya uwakili ili kupata mwitikio chanya kwa nchi za jumuiya ya Ulaya EU la kushughulikia changamoto zinazowakabilina maelfu ya watu wanaohatarisha maisha yao kutafuta usalama na maisha bora barani humo.

Katika kutatua tatizo la wahamiaji haramu na wakimbizi wanakutw na sintofahamu, UNHCR imesema imeandaa mapendekezo ikiwamo utafiti yakinifu,  operesheni za uokoaji, utafuataji wa makazi salama, vibali vya kusafiria kama sehemu ya usaidizi wa kibinadamu pamoja na kuunganishwa tena na familia.

Kufikia mwaka 2015, zaidi ya watafuta hifadhi 35,000 na wahamiaji wamewasili kwa njia ya boti barana Ulaya na ikiwa idadi ya vifo katika ajali ya jumamosi vitathibitishwa itafikisha idadi ya 1600. Mwaka 2014 takribani watu 219,000 walivuka Mediterranian na 3,500 walipoteza maisha.