Skip to main content

Miji ina nafasi muhimu katika kufikia SDGs: Graziano da Silva

Miji ina nafasi muhimu katika kufikia SDGs: Graziano da Silva

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Chakula na Kilimo Duniani, FAO, Jose Graziano da Silva amesema miji ina majukumu muhimu katika kumaliza njaa na kuboresha lishe.

Akihutubia mkutano wa mameya huko Milano, nchini Italia Bwana da Silva amesema hilo lawezekana wakati huu ambapo miji zaidi ya 100 kote duniani, imejitolea kuweka mifumo sawa na endelevu ya chakula maeneo ya mijini.

Amempongeza Meya wa mji wa Roma , Giuliano Pisapia na wenzake wa miji mengine kwa kusaini makubaliano ya sera ya chakula mijini.

Mkurugenzi huyo wa FAO amesema, kupitia makubaliano hayo, miji itajikita katika kanuni nne; kuhakikisha chakula na afya kwa wote; kukuza mfumo endelevu wa chakula ; kuelimisha umma kuhusu vyakula vilivyo na afya, na kupunguza taka .

Kwa mantiki hiyo, da Silva amesema miji itakuwa washikadau muhimu wa ajenda ya maendeleo endelevu, SDGs kufikia mwaka wa 2030.