Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNEP yapigia chepuo nguvu za sera na teknolojia katika kutunza mazingira

UNEP yapigia chepuo nguvu za sera na teknolojia katika kutunza mazingira

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Mpango wa Mazingira, Achim Steiner, amesema leo kuwa kupitishwa malengo 17 ya ajenda ya maendeleo endelevu na mabadiliko ya tabianchi ni mwanzo tu, na kwamba hadi yatimizwe, ulimwengu unapaswa kujiandaa kwa athari za mabadiliko ya tabianchi kwa mazingira.

Bwana Steiner amesema hayo kwenye kongamano la kimataifa kuhusu kuchukua hatua za kulinda mazingira, mjini Tokyo, Japan.

Mkuu huyo wa UNEP amesisitiza umuhimu wa nguvu za teknolojia na sera katika hatua zinazoweza kuchukuliwa sasa kimataifa katika utunzaji mazingira, akitolea mfano uzalishaji na matumizi ya nishati huishi na nishati rafiki kwa mazigira.

Amesema sekta ya nishati rafiki kwa mazingira inaingiliana vyema na malengo ya maendeleo endelevu, lakini hakuna maana ya kuendelea kuwekeza katika nishati huishi huku kukiendelea uharibifu wa nishati kwingineko.