Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hali ya fedha Umoja wa Mataifa sio nzuri: Takasu

Hali ya fedha Umoja wa Mataifa sio nzuri: Takasu

Ikiwa nchi wanachama hazitataoa michango yao kwa Umoja wa Mataifa kwa wakati hadi mwezi Novemba hali ya shirika hilo la kiranja wa nchi duniani itakuwa tete amesema Yukio Takasu ambaye ni msaidizi wa Katibu Mkuu kuhusu masuala ya utawala.

Bwana Takasu amewaeleza waandishi wa habari mjini New York hali ya shirika hilo kifedha akisisitiza kuwa Umoja wa Mataifa unategemea michango ya nchi wanachama katika kujiendesha ikiwamo kulipa mishahara.

(SAUTI TAKASU)

‘‘Kama nilivyotaja, kwa sasa dola bilioni moja haijalipwa na nchi wanachama. Hii ina maana gani? Tuna tatizo la mzunguko wa fedha wa dola milioni 73 kwa sasa. Umoja wa Mataifa una hifadhi dhaifu sana tuanouita mtaji wa fedha za kufanyia kazi wa dola milioni 150.’’

Amesema kwa sasa shirika hilo limeazima fedha ili kuendesha shughuIi zake mathalani za ulinzi wa maani.