Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNICEF yakaribisha pendekezo la kusitisha mapigano Sudan

UNICEF yakaribisha pendekezo la kusitisha mapigano Sudan

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF pendekezo la hivi karibuni la serikali ya Sudan na kikosi cha nchi hiyo la kusitisha mapigano.

Taarifa ya UNICEF inasema kuwa pendekezo hilo linakuja sambamba na wito wa mara kadha na mashirika mengine wa kutaka pande kinzani kusitisha mapigano ili kujali utu na usalama kwa watoto wakati wote pamoja na kuruhusu misaada ya kibidamu kufika katika maeneo ambayo hayafikiki kama vile milima ya Nuba, na jimboni Blue Nile.

UNICEF imesema kwa miaka minne maeneo haya yamekuwa hayafikiki na ukubwa wa mahitaji unafahamika kwa sehemu tu huku hali ikiwa inatisha matahalani Juba ambapo watoto zaidi ya 160,000 chini ya miaka mitano hawapatiwi chanjo.

Shirika hilo pia limesema watoto nchini Sudan inakabiliwa na surua, utapiamlo na kuharisha huku hali ya elimu ikiwa tete kutokana na machafuko takwimu zikionyesha kuwa watoto takribani miloni tatu waliopaswa kuwa shuleni hawajajiunga .

Chirstopher Boulerac ni msemaji wa UNICEF Geneva

(SAUTI CHIRSTOPHER)

‘’Kwa ujumla wataoto nchini Sudan wanaendelea kubeba mzigo mara mbili kama waathirika wakuu wa machafuko na ukosefu sugu wa maendeleo. Tumeanza kampeni ya chanjo miezi michache iliyopita, tunajiandaa kutoa chanjo kila mahali. Maeneo ambayo yalikuwa hayafikiki sasa tunafanya operesheni kuwalenga hao watoto’’