Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban ahoji iweje bajeti za kijeshi ni rahisi kupatikana kuliko za maendeleo

Ban ahoji iweje bajeti za kijeshi ni rahisi kupatikana kuliko za maendeleo

Mjadala wa wazi wa Baraza kuu la Umoja wa Mataifa umeanza leo kwenye makao makuu ya Umoja wa huo jijini New York, Marekani ukileta viongozi mbali mbali wan chi 193 wanachama wa chombo hicho ambacho mwaka huu kimetimiza miaka 70 tangu kuanzishwa kwake. Amina Hassan na maelezo zaidi.

(Taarifa ya Amina)

Nats

Hii ni video maalum iliyofungua pazia la mjadala huo utakaodumu kwa siku tatu, video ikielezea historia ya Umoja wa Mataifa uliozaliwa huko San Francisco miaka 70 iliyopita..

Nats..

Na ndipo Katibu Mkuu Ban Ki-moon akawasilisha ripoti ya mwaka ya utendaji wa umoja huo akisema kupitishwa kwa malengo ya maendeleo endelevu, SDGs, kumeweka bayana azma ya Umoja wa Mataifa ya kutokomeza umaskini na kuwa na maisha ya amani na utu kwa wote.

Hata hivyo amesema changamoto ni ufadhili wa kuwezesha maneno kuwa vitendo hasa suala la ufadhili akihoji..

“Dunia inaendelea kupoteza trilioni za fedha kwenye ununuzi wa vifaa vya kijeshi. Kwa nini ni rahisi kupata fedha za kuharibu watu na sayari ya dunia kuliko fedha za kuwalinda? Vizazi vijavyo vinatutegemea katika kuweka sawa vipaumbele vyetu.”

Mogens Lykketoft, Rais wa Baraza Kuu akafungua rasmi mjadala huo akisema hatua za pamoja zinatakiwa kutekeleza SDGs na hilo halina mjadala ..

(Sauti ya Mogens)

“Waheshimiwa, ni wakati sasa wa kufikia maamuzi ya kumaliza mizozo inayotia machungu, na kuanza kuwekeza zaidi kwenye maendeleo endelevu.”