Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza kuu laridhia azimio la ajenda 2030 kuhusu SDGs

Baraza kuu laridhia azimio la ajenda 2030 kuhusu SDGs

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa leo limeridhia rasimu ya azimio y ajenda ya maendeleo endelevu ya miaka 15 hadi mwaka 2030 inayolenga kusongesha mbele pale ambapo malengo ya maendeleo ya milenia, MDGs yanaishia. Taarifa zaidi na Assumpta Massoi.

(Taarifa ya Assumpta)

Azimio hilo namba A/69/L.85  lenye malengo 17 ya maendeleo endelevu, SDGs inatokana na mikutano tangulizi ambayo kwayo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon alipatiwa jukumu la kuitisha na kuibuka na maoni yenye lengo la kubadili dunia kwa maslahi ya wakazi wote.

Ban amesema leo wako tayari kukabidhi nyakara hiyo tayari kwa ajili ya kuridhiwa na viongozi wa nchi wanachama 193 wa Umoja wa Mataifa baadaye mwezi huu, ambapo amesema ajenda 2030 ina malengo ya juu kwa kuwa..

“Inaweka watu kama kitovu cha maendeleo. Inalenga kuchochea ustawi wa binadamu, amani, haki na dunia bora. Inasaka haki za watu wote na usawa wa kijinsia. Inazungumza na wakazi wa nchi zote na kutaka ushiriki wa kila mtu. Inalenga kutia hamasa na kuweka ubia sahihi baina ya nchi na wadau wote.”

Rais wa Baraza Kuu Sam, Kutesa akasema..

(Sauti ya Kutesa)

“Ajenda hii mpya ina matamanio makubwa, jumuishi na ni ya mabadiliko, inasaka kuona hakuna mtu anabakizwa nyuma.”