Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nimesononeshwa na hukumu ya mahakama ya Misri dhidi ya waandishi wa Aljazera: Ban

Nimesononeshwa na hukumu ya mahakama ya Misri dhidi ya waandishi wa Aljazera: Ban

Uamuzi wa mahakama ya Misri kuwahukumu waandishi watatu wa kito cha habari Aljazeera umepokelewa kwa masikitiko na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon

Siku ya Jumapili serikali ya Misri iliwahukumu Baher Mohamed, Mohamed Fahmy, Peter Greste na wawakilishi wengine wa kituo hicho cha habari wanaofanya kazi nchini humo.

Mwandishi raia wa Misri  Baher Mohamed na mwenzake raia wa Canada Mohamed Fahmy,  wamerejea jela maika mitatu baada ya kupatikana na hatia ya kuandika habari za kizushi licha ya kukata rufaa, huku raia wa Australia Peter Greste, aliyerudishwa nyumbani kwao mwezi Februari alihukumiwa bila kuwepo nchini Misri.

Taarifa ya msemaji wa Ban imesema  kiongozi huyo amehuzunishwa sana na uamuzi wa mahakama ya nchi hiyo na kukariri wito wake kwa kesi hizo  kutatuliwa kwa haraka na kwa kuzingatia wajibu wa Misri wa kulinda uhuru wa kujieleza na kujumuika.

Amesisitiza umuhimu wa kuheshimu haki za msingi kwa ajili ya mafanikio endelevu ya Misri .

Waandishi hao watatu awali walikamatwa mwaka 2013 na kuhukumiwa mwezi Juni mwaka jana  na mahakama ya nchi hiyo