Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uharamia Somalia wamulikwa, baraza la usalama lapitisha azimio.

UN Photo.
baraza-la-usalama

Uharamia Somalia wamulikwa, baraza la usalama lapitisha azimio.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa leo limepitisha azimio jipya kuhusu mapambano dhidi ya uharamia nchini Somalia ikiwa ni mara ya kwanza vitendo vya maharamia nchini humo vinajadiliwa katika baraza kama tishio la amani ya kimataifa na usalama katika ukanda huo.

Kadhalika azimio hilo linataka nchi kuhakikisha zinapambana na shughuli za uharamia hususani ni zile zinazofanywa katika nchi kavu kw akuzingatia ulinzi wa wanawake dhidi ya unyonyaji ikiwamo wa kingono.

Akihutubia baraza hilo mwakilishi wa Somalia katika Umoja wa Mataifa balozi Elmi Ahmed Duale  amesema nchi yake itatoa ushirkiano katika azimio hilo.

(SAUTI BALOZI ELMI)

Tunakaribisha mapendekezo , pamoja na  suluhisho la muda mrefu na mfupi lililopendekezwa katika azimio na tunawahakikishia ushirikiano katika mambo yote ikiwamo uharamia.