Skip to main content

Ban ataka nchi kuungana kupinga utowekaji wa watu

Ban ataka nchi kuungana kupinga utowekaji wa watu

Katibu Mkuu Wa Umoja wa Mataifa ametaka nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa kuungana katika  mkataba wa kimataifa wa kupinga vifungo vya siri, ikiwa ni wito wake wa maadhimisho ya nne ya siku ya kimataifa ya wahanga wanaotelekezwa, kutekwa au kutoweka.

Siku hiyo huadhimishwa mnamo Agosti 30 kila mwaka, Bwana Ban ametahadharisha kuwa idadi ya vitendo vya utoweshaji kukua.

Mwaka 2010 mkataba wa kimataifa wa kutangaza vitendo hivyo kuwa ni kinyume cha sheria uliwekwa katika utekelezaji licha ya kwamba vitendo hivyo bado hutekelezwa na baadhi ya nchi.

Hatma ya waathirika hao mara nyingi haifahamiki na huwa huteswa na kuogofya kuuliwa.

Katibu Mkuu amesema mwaka uliopita pekee timu mbili maalum za wataalamu wa Umoja wa Mataifa ambao zinashughulikia suala la kutoweka yalipokea  maombi 246 kutoka kwa familia kote duniani zikitaka kuchukuliwa kwa hatua za dharura.