Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nchi zatakiwa kuungana katika kupinga majaribio ya nyuklia

Nchi zatakiwa kuungana katika kupinga majaribio ya nyuklia

Katika  ujumbe wake kuhusu siku ya kimataifa ya kupinga majaribio ya nyuklia, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amezitaka nchi kuungana katika makataba wa kimataifa wa kupinga silaha za nyukilia ili mkataba huo utekelezeke.

Katibu Mkuu amekaribisha upigwaji marufuku wa hiari wa majaribio ya nyuklia uliotekelezwa na mataifa yanayotengeneza silaha hizo lakini akasema haitoshi

Tangu matumizi ya kwanza ya nyuklia mnamo mwaka 1945, zaidiya majaribio 2000 yamefanyika sehemu tofauti duniani na kusababisha madhara kadhaa ikiwamo saratani huku baadhi ya jamii bado zikiwa na majeraha ya madhara.

Katika ujumbe wake ikiwa ni maadhimisho ya tano, Ban amesema njia bora kuwaenzi wahanga wa majaribio yaliyopita ni kuzuia vitendo hivyo visifanyike.

Amesema ikiwa ni takribani miongo miwili tangu kuanzishwa kwa mkataba wa kupinga silaha za nyuklia , muda mrefu umepita bila utekelezaji.

Bwana Ban amesema kuupa meno mkataba huo ni hatua muhimu, kuelekea katika dunia isiyo na nyuklia.