Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vijana duniani wajadili maendeleo Tanzania

Vijana duniani wajadili maendeleo Tanzania

Mkutano wa dunia wa vijana kuhusu maendeleo ya kundi hilo unafanyika mjini Dar es salaam nchini Tanzania kuanzia hii leo ambapo vijana washiriki kutoka mataifa mbalimbali watafundishwa kwa mifano halisi namna ya kutumia fursa.

Katika mahojiano na idhaa hii mwenyekiti wa taasisi ya kimataifa ya ushirika wa vijana IYF Tanzania,  Emmanuel Ngoga amesema mkutano huo wa siku nne utawaleta pamoja  zaidi ya vijana 3000, kubadilishana uzoefu na kupeana mawazo na akafafanua dhima ya kambi.

(SAUTI EMMAUEL)

Kambi hii inafanyika ikiwa ni juma moja baada ya Umoja wa Mataifa kuadhimisha kwa mara ya kwanza kwanza  siku ya kimataifa ya ujuzi kwa vijana ambapo Katibu Mkuu Ban Kin- moon amesema elimu zaidi kwa vijana inahitajika kwani vijana milioni 75 hawako shuleni na hivyo wanakosa ujuzi.