Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tuzisaidie nchi za visiwa vidogo kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na usalama:Ban

Tuzisaidie nchi za visiwa vidogo kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na usalama:Ban

Baraza la Usalama leo limeendesha mjadala wa wazi kuhusu changamoto za amani na usalama kwa nchi za visiwa vidogo zinazoendelea (SIDS) ambapo imeelezwa kuwa mabadiliko ya tabia nchi na uhalifu wa kimataifa ni moja ya changamoto kuu kwa nchi hizo.

Akihutubia baraza hilo Katibu Mkuu Ban Ki- moon ameitaka jamii ya kimataifa kuisaidia SIDS kukabiliana na madhara ya mabadiliko ya tabia nchi na kuwezesha maendeleo endelevu.

Kuhusu uhalifu unaovuka mipaka na kuathiri nchi hizi Ban anataja baadhi ya hatua zinazochokuliwa.

(SAUTI BAN)

‘‘Ofisi ya Umoaj wa Mataifa ya madawa na uhalifu UNODC, kupitia mpango wa kudhibiti uhalifu baharini imejikita katika usafirishaji haramu wa madawa aina ya Heroine, wanadamu, wanayama pori na samaki.’’

Kwa upande wao wawakilishi wa nchi za visiwa vidogo vinavyoendelea wamesema uhalifu wa kupangwa umefikia hatua mbaya hususani kwa kutumia mtandao wa intaneti na hivyo kuitaka jumuiya ya kimataifa kushirikiana nao katika makbiliano.