Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tutumie urafiki kukuza amani na mawelewano: Ban

Tutumie urafiki kukuza amani na mawelewano: Ban

Ikiwa leo ni Siku ya Kimataifa ya Urafiki,  Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Kin-moon amesema dhana hii ambayo ni wazo la shujaa mwenye maono laweza kujenga madaraja miongoni mwa watu na kuchochea amani duniani.

Katika ujumbe wake wa kuadhimisha siku hii Bwana Ban amesema urafiki ni muhimu katika kukabiliana na ubaguzi, uovu na ukatili ambavyo huchochea machafuko na mauaji yanayowatesa mamilioni ya watu . Ametaka watu kuwa karibu na kukuza heshima na maelewano katika dunia.

Nchini Uganda baadhi ya raia wanazungumzia umuhimu wa urafiki kama walivyomweleza mwandishi wetu John Kibego

(VOX POP)

Mbeba maono ya siku ya kimataifa ya urafiki ni Dk Ramón Bracho, raia wa Paraguay.