Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tanzania na mikakati ya kudhibiti homa ya ini

Tanzania na mikakati ya kudhibiti homa ya ini

Madhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Kupinga Ugonjwa wa Homa ya Ini kwa kitaalamu Hepatitis yamefanyika Julai 28 ambapo Shirika la Afya Uliwmenguni(WHO) ambalo limeratibu maadhimisho hayo limetoa wito kwa nchi wanachama kuhakikisha matibabu dhidi ya homa hiyo hatari.

Joseph Msami amezungumza na Dk. Janeth Mgamba ambaye ni  ni Mkurugenzi msaidizi wa kitengo cha kudhibiti magonjwa ya milipuko nchini Tanzania. Kwanza ameanza kwa kumuuliza ugonjwa huo ni nini hasa?