Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ufadhili dhidi ya malaria wafikia kiwango kipya

Ufadhili dhidi ya malaria wafikia kiwango kipya

Vita dhidi ya malaria ni mfano bora katika utekelezaji wa malengo ya maendeleo ya milenia, amesema leo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon, wakati wa mkutano maalum kuhusu malaria uliofanyika mjini Addis Ababa, nchini Ethiopia, wakati wa kongamano la tatu la kimataifa kuhusu ufadhili kwa maendeleo.

Ban ameongeza kwamba ajenda mpya ya manedeleo endelevu itawezesha kutokomeza ugonjwa huo.

Katika mahojiano na Redio ya Umoja wa Mataifa, Waziri wa Fedha wa Kenya, Henry Rotich, ameeleza umuhimu wa kupambana na malaria ili kuwezesha maendeleo..

(Sauti ya Henry Rotich)

Lengo la Shirika la Afya Duniani WHO pamoja na Ubia kwa kutokomeza Malaria ni kupunguza visa vya malaria kwa asilimia 90 ifikapo mwaka 2030.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa WHO Margareth Chan ametangaza uzinduzi wa mfumo mpya wa ufadhili kwa vita dhidi ya malaria, unaozingatia juhudi za kitaifa.