Mkuu wa UN Women azuru Sudan Kusini

7 Julai 2015

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya wanawake, UN Women, Phumzile Mlambo-Ngcuka, anafanya ziara ya siku mbili nchini Sudan Kusini, kuanzia leo Julai 7 hadi Julai 8, 2015.

Akiwa mjini Juba, Dkt. Mlambo-Ngcuka atakutana na raia wa Sudan Kusini, Salva Kiir Mayardit na mawaziri, maafisa wengine wa ngazi ya juu serikalini, wawakilishi wa mashirika ya umma, ukiwemo mtandao wa wanawake wa Sudan Kusini kwa ajili ya amani, SSWPN na mengineyo.

Dhamira kuu ya ziara ya mkuu huyo wa UN Women ni kuendelea kuonyesha mshikamano wake na wanawake na wasichana nchini humo wakati vita vikiendelea, kufuatia ziara yake ya awali alipokutana nao. Anatarajiwa pia kutumia fursa hii kutoa wito wa ujumuishaji na amani endelevu na kuinua nafasi ya wanawake na kuwawezesha kushiriki katika ulinzi wanawake na wasichana na ujenzi wa amani.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter