Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNAMA yaelezea mshikamano na mashirika ya umma na wanahabari Afghanistan

UNAMA yaelezea mshikamano na mashirika ya umma na wanahabari Afghanistan

Mjumbe wa Umoja wa Mataifa Afghanistan, Nicholas Haysom, amekutana leo mjini Kabul na wanaharakati wa umma na waandishi wa habari ili kuwasikiliza wakielezea hofu yao kuhusu vitisho ambavyo wamepokea hivi karibuni kutoka makundi yenye silaha kutoka nje ya nchi.

Bwana Haysom amesema uandishi habari thabiti na huru, pamoja na kunawiri kwa wanaharakati wa umma ni muhimu kwa ustawi wa demokrasia. Amesema taifa la Afghanistan linaweza kujivunia sekta zake za uandishi habari na mashirika ya kiraia, lakini ufanisi huo unapaswa kulindwa.

Ameongeza kuwa mamlaka za Afghanistan zinapaswa kuchukua hatua stahiki ili kuwalinda wana taaluma ambao wanakumbwa na vitisho, huku akilaani vitisho vya hivi karibuni na kuorodheshwa kwa wanahabari na wawakilishi wa mashirika ya kiraia kama walengwa wa kupewa ‘adhabu’ kwenye mitandao ya kijamii.