Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Miaka 70 ya UM, tuamue mustakhbali sahihi: Ban

Miaka 70 ya UM, tuamue mustakhbali sahihi: Ban

Leo ni miaka 70 tangu kuanzishwa kwa Umoja wa Mataifa ambapo Katibu Mkuu wa Umoja huo Ban Ki-Moon amesema maadhimisho haya yanafanyika dunia ikiwa inakabiliwa na changamoto ya kuafikiana mustakhbali wa sayari hiyo. Taarifa zaidi na Assumpta Massoi.

(Taarifa ya Assumpta)

Miaka 70 iliyopita katika hali iliyoonekana kuwa ni ngumu zaidi ya maelewano baada ya vita vikuu vya pili vya dunia, mataifa 50 yalikutana huko San Francisco nchini Marekani na kukubaliana katiba ya kuanzisha Umoja wa Mataifa kwa lengo la kuendeleza amani duniani, ustawi na haki za binadamu.

Akizungumzia siku hii ambayo maadhimisho  yanafanyika San Francisco Katibu Mkuu Ban Ki-moon amesema…

(Sauti ya Ban)

Kuadhimisha siku hii tunakutana tena pale umoja wa mataifa ulipozaliwa, mwaka huu viongozi wa dunia wataamua mustakhbali ili kumaliza umaskini uliokithiri na kudhibiti mabadiliko ya tabianchi. Tunataka mwaka 2015 uwe mwaka wa utekelezaji kwa binadamu na sayari yetu.”

Baada ya kuasisiwa na mataifa 50 mwaka 1945, hii leo Umoja wa Mataifa umekua na unaundwa na nchi wanachama 193.