Skip to main content

Baraza la Usalama liache kupooza, lichukue hatua dhidi ya ISIL: Mtaalamu

Baraza la Usalama liache kupooza, lichukue hatua dhidi ya ISIL: Mtaalamu

Mtaalamu Maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu kukuza na kulinda haki za binadamu na uhuru wakati wa kukabiliana na ugaidi, Ben Emmerson leo amewasilisha ripoti yake mbele ya baraza la haki za binadamu huko Geneva, Uswisi inayoangazia ukiukwaji mkubwa unaofanywa na kikundi cha kigaidi kinachotaka kuunda dola la kiislamu ISIL ama Da'esh, na umuhimu wa  kuwepo kwa uwajibikaji. Taarifa kamili na Grace Kaneiya..

Taarifa ya Grace

Katika ripoti yake amesema baraza la usalama limeonyesha kushindwa kwa hali ya juu kuchukua hatua madhubuti za utekelezaji wa sheria ya kimataifa dhidi ya ISIL na kuwalinda raia walio katika maeneo yanayoshikiliwa na ISIL, na azimio lililopitishwa na baraza la usalama siyo suluhu bali

(Sauti ya Ben Emmerson)

"Maazimio kama haya hayakomeshi ugaidi unaotekelezwa na ISIL. Ni ishara ambayo hata haigusi uso wa tatizo hili. Ukweli ni kwamba kwa kupooza kwa taasisi hii hata katika hali tete kama hii, Baraza limeonyesha kushindwa kutekeleza mamlaka iliyopatiwa na katiba ya Umoja wa Mataifa."

Bwana Emmerson amesema kwamba Baraza la Usalama lina wajibu wa kuchukua hatua kivitendo, na kutokana na ripoti ya mauaji ya kimbari wanachama wote wa Baraza pia sasa wana wajibu maalum wa kuchukua hatua ya kuzuia uhalifu huu mkubwa wa kimataifa.