Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chanjo ya homa ya manjano kutolewa mara moja: WHO

Chanjo ya homa ya manjano kutolewa mara moja: WHO

Baraza Kuu la Shirika la Afya ulimwenguni WHO ambalo limemaliza vikao vyake hii leo mjini Geneva limepitisha maazimio muhimu katika kukabiliana na changamoto za afya ikiwamo chanjo ya homa ya manjano ambapo badala ya kurudia mara kadhaa limependekeza chanjo hiyo itolewe mara moja. Taarifa kamili na Grace Kaneiya..

(TAARIFA YA GRACE KANEIYA)

Taariofa ya maazimio hayo inasema kuwa kundi la wataalamu wa chanjo wamependekea kuwa chanjo mara moja inatosha kudumu kwa kipindi kirefu dhidi ya ugonjwa na hivyo kurudia chanjo hiyo si lazima.

Kundi hilo la wataalamu limeongeza kuwa kwa mujibu wa sheria za afya za kiamataifa za mwaka 2005 , chanjo yaweza kuhitajika ikiwa msafriri anatoka katika eneo ambalo lina hatari kubwa ya maambukizi ya homa ya manjano. Utekelezaji wa utaratibu huo mpya unatarajiwa kuanza mwaka ujao.

Katika hatua nyingine WHO imependekeza kuweka msisitizo katika lishe kulingana na makubaliano ya baraza hilo mwaka 2012 ambapo nchi wanachama walitakiwa kuhakikisha lishe bora kwa mama na watoto ili kukabiliana na utapiamlo.