Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tanzania yataja mikakati ya matumizi sahihi ya nishati ya gesi:

Tanzania yataja mikakati ya matumizi sahihi ya nishati ya gesi:

Mkutano wa kila mwaka kuhusu nishati endelevu unaendelea mjini New York ambapo hii leo Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Jan Eliasson amefungua majadiliano ya mawaziri wa nishati kutoka sehemu mbalimbali duniani akisema nishati endelevu ni dhana muhimu katika ukuaji wa kiuchumi, kijamii na ulinzi wa mazingira.

Bwana Eliasson amesema kuwa lengo ni kuleta mabadiliko katika sekta kama kilimo, na pia kubadili maisha ya wanajamii.

Katika mahojiano na idhaa hii mwakilishi wa Tanzania katika mkutano huo , Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushi anaeleza ujumbe wa nchi yake katika mkutano huo.

(SAUTI MUSHI)

Kadhalika akataja mikakati ya kuendeleza gesi iliyogunduliwa nchini humo ili kuwanufaisha wananchi.

(SAUTI MUSHI)