Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ufanisi wa matumizi ya rasilimali ni muhimu katika mapinduzi mapya ya viwanda Asia Pacific: ripoti

Ufanisi wa matumizi ya rasilimali ni muhimu katika mapinduzi mapya ya viwanda Asia Pacific: ripoti

Upotevu wa matumizi ya rasilimali katika mataifa ya Asia-Pacific unadidimiza uwezo wa nchi hizo kukuza uchumi wake katika siku za usoni , lakini kuna uwezekano mkubwa wa ukuaji unaozingatia matumizi madogo ya cabon imesema ripoti ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Mazingira(UNEP) iliyotolewa kwenye kongamano la kwanza la mawaziri wa mazingira wa Asia Pacific.

Ripoti hiyo ambayo imetoa wito wa kuwa na mapinduzi mapya ya viwanda kuchagiza afya za watu kwa matumizi madogo ya rasilimali , pia imeonya kuwa eneo la Asia Pacific haliwezi kutegemea tuu kuporomoka tu kwa gharama za mali asili kwa ajili ya kukuza uchumi wake siku za usoni.

Mipango endelevu inahitajika kwa ajili ya eneo hilo lakini inahitaji ufadhili wa kiasi cha dola trilioni 2.5 kwa mwaka kuhakikisha uwekezaji endelevu wa maendeleo imesema ripoti hiyo ya UNEP.

Kwa mujibu wa mkurugenzi mtendaji wa UNEP Achim Steiner, maendeleo makubwa ya kiuchumi katika eneo hilo yameinua maisha ya mamilioni ya watu kutoka kwenye umasikini lakini bado hakuna usawa, mabadiliko ya tabianchi yanaendelea kuwa tishio na kama inavyoashiria ripoti upotevu wa matumizi ya rasilimali imekuwa tatizo tangu kati ya 1990 na 2010.