Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR, OHCHR, IOM yataka waliokwama Andaman wasaidiwe:

UNHCR, OHCHR, IOM yataka waliokwama Andaman wasaidiwe:

Wakuu wa Mashirika ya Kuhudumia Wakimbizi(UNHCR), Kamishina Mkuu wa Haki za Binadamu, Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Uhamiaji(IOM) na Mwakilishi Maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Uhamiaji, wamewataka viongozi wa Indonesia, Malaysia na Thailand kuwalinda wahamiaji na wakimbizi waliokwama kwenye meli katika ghuba ya Bengali na bahari ya Andaman.

Viongozi hao António Guterres, Zeid Ra’ad Al Hussein, William L. Swing, na Peter Sutherland, wamezitaka serikali za Indonesia na Malaysia kusaidia wahamiaji hao na wakimbizi kutoka kwa usalama kwenye meli, kutoa kipaumbele katika kuokoa maisha yao, kulinda haki za binadamu na kuheshimu utu wa mtu.

Matukio ya hatari ya karibuni kwenye ghuba ya Bengali na bahari ya Andaman yakihusisha wahamiaji na wakimbizi wa Rohingya na wengine kutoka Bangladesh na Myanmar yanathibitisha kwamba watu wasiojiweza kote duniani wanasafiri wakitafuta usalama na utu, wakikimbia mauaji, ubaguzi na mateso. Nasafari wanazozichua za hatari ziwe ni za ardhini, baharini au angani zimekuwa ni msukosuko wa kimataifa.

Kusini Mashariki mwa Asia zaidi ya watu 88,000 wamefanya safari hizo za hatari kupitia baharini mwaka 2014 wakiwemo watu 25,000 ambao wamewasili robo ya mwaka huu pekee, huku wengine 1000 wamepoteza maisha katika safari hizo.