Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNRWA kunufaika na msaada kutoka Ujerumani

UNRWA kunufaika na msaada kutoka Ujerumani

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi wa Kipalestina UNRWA litanufaika kwa mchango wa Euro milioni 80 kutoka kwa Ujerumani nchi ya pili kwa kiwango kikubwa cha michango kwa shirika hilo.

Taarifa ya UNRWA inasema kuwa Ujerumani imetangaza kiasi hicho cha fedha ambazo ni kwa ajili ya kuwezesha mpango wa malazi kwa wakimbizi walioko Gaza.

Shirika hilo linasema kuwa hadi sasa limepeleka ufadhili wa kutosha kujenga makazi 200 kati ya 1961 ya wakimbizi wa Palestina ambao makazi yao yaliharibiwa kabisa. Mkurugenzi wa operesheni za UNRWA Gaza, Robert Turner ameshukuru Ujerumani kwa msaada huo na kuongeza kuwa miezi nane baada ya machafuko wakati wa majira ya kiangazi kumalizika hali inasalia tete Gaza na watu wa eneo hilo wanahitaji misaada zaidi ya dharura.

Mwaka 2014 Ujerumani ilikuwa ilikuw anchi ya tano kwa kwa kuchangua UNRWA kwa kiasi cha dola milioni 79.