Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mashambulio ya anga na ardhini Yemen yamsikitisha Ban

Mashambulio ya anga na ardhini Yemen yamsikitisha Ban

Ripoti ya  kuendelea kwa mashambulizi ya anga na ya ardhini huko Yemen huku yakilenga raia wasio na hatia zimemsikitisha kwa kiasi kikubwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon.

Taarifa ya msemaji wa Umoja wa Mataifa imemkariri Ban akisema kuwa hali hiyo inaendelea ambapo majengo ya umoja huo, miundombinu ya kiraia ikiwemo hospitali na maghala ya kuhifadhi misaada ya kibinadmu inashambuliwa jambo ambalo amesema halikubaliki na kinyume na sheria za usaidizi wa kibinadamu za kimataifa.

Amerejelea tena wito wake kwa pande husika kwenye mzozo wa Yemen kuingia makubaliano ya kusitisha mapigano au kuruhusu misaada ya kibinadamu isambazwe wakati huu ambapo uhaba wa mafuta unatishia mgao wa misaada.

Zaidi ya watu 1,200 wameuawa na wengine 300,000 wamekimbia makazi yao katika kipindi cha wiki sita zilizopita kutokana na mashambulizi hayo huko Yemen.