Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNESCO yafungua shule ya tatu kwa wakimbizi wa ndani Iraq:

UNESCO yafungua shule ya tatu kwa wakimbizi wa ndani Iraq:

Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu , Sayansi na Utamaduni UNESCO na washirika wake leo wamesherekea pamoja na wanafunzi na waalimu kufunguliwa kwa shule mpya ya Migrant Birds maalumu kwa ajili ya wakimbizi wa ndani kwenye kambi ya Al-Souq Al Asry mjini Basrah, Iraq.

Kufunguliwa kwa shule hiyo kambini Al Souq Al Asry kunafuatia kufunguliwa pia kwa shule ya sekondari ya Baharka na ya Dawodiyah ambazo pia ni mafanikio makubwa kwa juhudi za UNESCO za kutoa elimu bora kwa watoto na barubaru kwenye jamii za wakimbizi wa ndani na kuhakikisha fursa sawa ya elimu kwa wasichana na wavulana.

Hafla ya ufunguzi wa shule hiyo imefanyika mbele ya maafisa wa serikali na elimu mjini Basrah, na pia kuhudhuriwa na wanafunzi, wazazi, waalimu, pamoja na wajumbe wa mashirika yasiyo yakiserikali NGO’s na jumuiya ya kimataifa . Hafla hiyo ilijumuisha ziara ya shule nzima, na maandalizi mbalimbali kama ngoma zilizoandaliwa na wanafunzi ikiwemo pia nyimbo na usomaji wa mashairi.

Familia 270 270 ambazo ni jumlya ya watu 24000 wanaishi kambini Al-Souk Al-Asari , hivyo kufunguliwa kwa shule hii leo kutasaidia wanafunzi wengi kuendelea na elimu.