Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vijana wana wajibu mkubwa katika kuchagiza Amani na kukabiliana na itikadi kali:Ban

Vijana wana wajibu mkubwa katika kuchagiza Amani na kukabiliana na itikadi kali:Ban

Tunaanzia Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York ambako Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amesema jukumu la vijana ni kubwa katika kuchagiza amani na kukabiliana na itikali na misimamo mikali. Flora Nducha na taarifa kamili.

(TAARIFA YA FLORA NDUCHA)

Mjadala huo umeongozwa na mwana mfaleme wa Jordan , Hussein Bin Abdullah II, na umejikita katika mada ya kupambana na ghasia zitokanazo na itikali kali na kuchagiza amani.

Akizungumza kwenye mjadala Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-Moon amesema jukumu la vijana liko katika kitovu cha Amani ya kimataifa na usalama , lakini vijana wengi wanakuwa wahanga wa vitendo vya kikatili vitonavyo na misimamo mikali akitolea mfano mashambulizi ya karibuni kwenye chuo kikuu cha Garisa nchini Kenya , lakini amesema wa uwezo, fikira na mtazamo wa kuweza kubadili hali hii..

(BAN CLIP)

“Wakati baadhi ya vijana wanatekelza uhalifu walio wengi wanalilia amani hasa katika maeneo ya vita, mara kwa mara tunawaona vijana wakibeba mzigo wa ghasia zitokanazo na misimamo mikali. Wana udhanifu, ubunifu na uwezo wa kimtandao, wanelewa machungu ya vita na mahitaji ya amani.”

Naye mwana mfalme wa Jordan, Hussein Bin Abdullah II ambaye ndiye mwenyekiti wa mjadala huo amesema..

(PRINCE HUSSEIN BIN ABDULLAH CLIP)

“ Kuna maongezi kwamba vijana ni kundi lililotengwa lakini niruhusuni niseme sio kundi lililotengwa bali linalolengwa. Wanalenwa kutokana na umuhimu wa umri wao , kujiamini kwao na uwezo wao wa kuleta mabadiliko duniani."