Sasa si wakati wa kujitoa kwenye harakati dhidi ya Ebola: Nabarro
Wakati Benki ya dunia ikitangaza kuzipatia Sierra Leone, Guinea na Liberia jumla ya dola Milioni 650 kwa kipindi cha miezi 12 hadi 18 ijayo ili kujikwamua kutoka athari za mlipuko wa Ebola, Mjumbe maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Ebola David Nabarro amesema mlipuko wa Ebola bado unaendelea hivyo juhudi za pamoja ziendelee. Taarifa ya Amina Hassan inafafanua zaidi.
(Taarifa ya Amina)
Suala la Ebola limekuwa ajenda ya vikao vya leo asubuhi vya mikutano ya Benki ya dunia huko Washington DC, vikao vilivyohudhuriwa pia na Katibu Mkuu Ban Ki-moon na marais wa nchi tatu zilizoathirika zaidi na Ebola, Liberia, Guinea na Sierra Leone.
Wote wamesisitiza umuhimu wa kuendeleza jitihada za pamoja kumaliza mlipuko huo huku Bwana Nabarro akisema mlipuko unaendelea kwani hadi sasa kuna visa vipya vinaibuka.
(Sauti Nabarro)
Ili kufanya hivyo sote ni lazima tuongeze maradufu juhudi zetu na serikali na wananchi hasa wiki zinazokuja kabla mvua hazijaimarika. Hatuwezi! Hatuwezi! kujiondoa wakati hu hatari zaidi. Napazia wito wa maraia hebu tuhakikishe tunasaka mbinu za kutokomeza mlipuko huu wiki zijazo.”
Wakati huo huo dola Milioni 650 ambazo Benki ya dunia itazipatia Guinea, Liberia na Sierra Leone zinafanya kiasi cha fedha kilichotolewa na taasisi hiyo kwa harakati za kujikwamua kufikia zaidi ya dola bilioni Moja na Nusu.