Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ebola yasababisha wengine kunyanyapaliwa na kufukuzwa kwenye makazi

Ebola yasababisha wengine kunyanyapaliwa na kufukuzwa kwenye makazi

Kunyanyapaliwa na kufukuzwa makwao kwa watu walioambukizwa ugonjwa wa Ebola au hata wale wanoshukiwa kuwa na huo nchini Sierra Leone, kumesababisha kuanzishwa kwa mradi wa makazi ya muda kupitia mradi wa matokeo ya haraka, QIPS.

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa Kuhusu Ebola (UNMEER) unafadhili miradi hiyo kwa ajili ya siyo tu kuwahifadhi watu hao balipia kuwahudumia chini ya karantini ya siku 21 ili pia kuzuia maambukizi zaidi ya ugonjwa huu katika jamii .

Je hali inakuwa vipi hadi wanafika kwenye makazi hayo? Ungana na Joseph Msami kwenye makala hii..