Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mzozo wa Yemen, mamia wakimbilia pembe ya Afrika

Mzozo wa Yemen, mamia wakimbilia pembe ya Afrika

Wakimbizi  900 wamewasili katika nchi mbali mbali za pembe ya Afrika wakikimbia mapigano yanayoendelea huko Yemen.

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa, UNHCR limesema watu hao wanavuka ghuba ya Aden kueleka ukanda huo wa pembe ya Afrika, ikiwa ni tofauti na awali ambapo watu wengi walikuwa wanakimbilia Yemen.

Mathalani UNHCR imesema katika siku 10 zilizopita wakimbizi zaidi ya 300 kutoka Yemen wameingia mji wa Obock nchini Djibouti.

Huko bandari ya Bossaso iliyoko Puntiland wakimbizi 582 wamewasilii na wakiwemo wasomali, wayemen na hata waethiopia na raia wa Djibouti.

UNHCR imesema wakimbizi hao watapatiwa chakula, maji na kwamba watakaguliwa afya zao.