Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Umoja wa Mataifa wakaribisha ushindi wa Iraq jimboni Tikrit

Umoja wa Mataifa wakaribisha ushindi wa Iraq jimboni Tikrit

Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Iraq . Ján Kubiš, amekaribisha ushindi wa hivi karibuni wa vikosi vya  usalama vya Iraq katika kuukomboa mji wa Tikrit kutoka mikononi mwa ISIL na vikundu vingine vyenye silaha.

Bwana Kubiš amenukuliwa akisema kuwa huo ni ushindi wa watu wote wa Iraq na kuongeza kuwa Umoja wa Mataifa uko tayari kusaidia mamlaka za  kikanda na kitaifa katika kutoa misaada kwa maelfu ya raia waliopoteza makazi.

Amesema usalama wa raia lazima ulindwe kwa kuzingatia haki za binadamu kanuni na sheriaya kibinadamu huku akitaka serikali kuhakikisha kuwa wakazi wote wa Tikrit waliokimbia makazi yao warejee majumbani kwao salama na mahitajia yao kibinaadamu yanayohitajika yafikishwe bila kuchelewa.