Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Japan na Uholanzi zajiunga na mradi wa UNISDR wa miji inayostahimili majanga:

Japan na Uholanzi zajiunga na mradi wa UNISDR wa miji inayostahimili majanga:

Nchi mbili zilizo katika msitari wa mbele kwenye juhudi za kimataifa za kupunguza hatari ya majanga leo zimeungana na ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kupunguza hatari za majanga (UNISDR) katika mradi wa ushirikiano wa kuimarisha uwezo wa miji kustahimili majanga.

Wizara ya miundombinu na mazingira ya Uholanzi, jumuiya ya biashara ya Japan inayowakilisha makampuni madogo na makubwa 119 na UNISDR wameafikiana kuanzisha njia itakayokuwa daraja baina ya uwezo wa kustahimili majanga na huduma zinazohitajika katika miji kufikia lengo hilo.

Katika taarifa yao ya pamoja ya ushirika wadau hao watatu wataunganisha miji, wadau wa maendeleo na biashara ili kubadilishana mawazo, huduma na uwezo wa umma na sekta binafsi kuchagiza hatua za kupunguza hatari ya majanga mijini.

Bi Margareta Wahlström, mkuu wa head of UNISDR, amesema ni bayana kwamba hatari mijini inaongezeka haraka kuliko uwezo wa kukabiliana nayo. Hivyo ni muhimu kuhakikisha suluhu, nyenzo na njia za kujenga uwezo wa kuhimili majanga sio tuu zipo bali zinapatikana.