Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban ampongeza mfalme Mswati III kwa kukabiliana na umasikini na ukimwi

Ban ampongeza mfalme Mswati III kwa kukabiliana na umasikini na ukimwi

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa amekutana na mfalme Mswati III kandoni mwa mkutano wa kupunguza hatari ya majanga unaonedelea Sendai Japan.

Katika mkutano wao Ban amempongeza mfalme na utawala wa Swaziland kwa juhudi kubwa za kushughulikia matatizo ya kutokuwepo usawa wa kipato, kupunguza umasikini na vita dhidi ya HIV/ ukimwi nchini humo.

Viongozi hao pia wamejadili ajenda ya maendeleo endelevu , na pia hali ya nchi jirani ya Lesotho.