Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

FAO yasaidia wakulima wadogo wadogo barani Afrika

FAO yasaidia wakulima wadogo wadogo barani Afrika

Shirika la Chakula na Kilimo FAO limeridhika na mradi ulioanzishwa miaka mitatu iliyopita barani Afrika, kwa lengo la kuimarisha usalama wa chakula pamoja na kuwezesha wakulima wadogo wadogo.

Mradi huo umeiiga mfano wa Brazil ambayo ni nchi iliyofanikiwa katika vita dhidi ya njaa na umaskini, na mradi huo umetekelezwa katika nchi tano ikiwemo Msumbiji, Malawi na Ethiopia.

FAO imesaidia serikali za nchi hizo kuwapatia watoto mlo shuleni, ikununua vyakula kwa wakulima wadogo wadogo kuliko kuvinunua kwenye masoko ya jumla. Kwa mujibu wa FAO, mkakati huu umeweza kuendeleza ukulima vijijini na kuimarisha uzalishaji wa wakulima hawa.

Florence Tardenac ni mtalaam wa FAO.

"Mradi huu unaleta matumaini kwa sababu kwa upande moja unatimiza lengo la kuimarisha chakula cha watoto shuleni. Lakini pia ni uzoefu mzuri kwa wakulima wadogo wadogo katika kuuza bidhaa zao kwenye masoko makubwa ambayo yana kiwango cha juu cha ubora".

FAO inatarajia kuendesha tathmini ya mradi huo ili kuangalia jinsi ya kupanua utekelezaji wake kwenye nchi zingine na maeneo mengine.