Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Feltman aanza ziara Myanmar, kisha Sri Lanka

Feltman aanza ziara Myanmar, kisha Sri Lanka

Msaidizi wa Katibu Mkuu kuhusu masuala ya kisiasa, Jeffrey Feltman, yumo safarini kuelekea nchini Myanmar, ambako anatarajiwa kushiriki katika warsha ya Umoja wa Mataifa na shirika la nchi za Kusini Mashariki mwa Asia, ambayo inaangazia ushirikiano katika kuunga mkono Taasisi ya Asia kuhusu Amani na Maridhiano.

Hii ni ziara ya pili ya Bwana Feltman, baada ya ile aliyoifanya mwaka 2014 wakati wa mkutano mkuu wa Asia.

Msemaji wa Katibu Mkuu Stephane Dujarric amesema baada ya ziara yake Myanmar, Bwana Feltman atasafiri kwenda Sri Lanka

“Huko anapanga kukutana na maafisa wa ngazi ya juu wa serikali ya Sri Lanka, vyama vya kisiasa na makundi ya kijamii. Hii itakuwa ziara yake ya kwanza Sri Lanka, na anatazamia kujadili na viongozi wa Sri Lanka masuala kadhaa muhimu.