Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Afya ya wanawake izingatiwe katika ajenda ya maendeleo:UM

Afya ya wanawake izingatiwe katika ajenda ya maendeleo:UM

Katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa, mjini New York, idara ya maswala ya kijamii ya Umoja huo pamoja na Shirika la kifalme la amana ya kimataifa ya sayansi, RASIT, imeandaa mjadala maalum kuhusu uhusiano baina ya afya ya wanawake na maendeleo. Taarifa zaidi na Joshua Mmali.

(Taarifa ya Joshua)

Licha ya mafanikio katika afya ya wanawake, bado mamilioni ya wasichana na wanawake duniani kote hawapati dawa, chanjo na huduma za afya zinazotakiwa, kwa mujibu wa idara ya maswala ya kijamii ya Umoja wa Mataifa, huku ukosefu wa usawa wa kijinsia ukikumba afya ya wanawake.

Hata hivyo, suluhu mbadala linaweza kupatikana ili kuboresha hali kupitia teknolojia mpya na endelevu. Washiriki wa kongamano linalofanyika leo mjini New York wamesisitiza umuhimu wa kuzingatia suala la afya ya wanawake katika ajenda ya maendeleo endelevu, baada ya mwaka 2015.

Princess Nisreen El-Hashemite ni mkurungenzi wa RASIT.

(Sauti ya El-Hashemite)