Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Maendeleo yoyote ya jamii yajali utu wa binadamu: Ban

Maendeleo yoyote ya jamii yajali utu wa binadamu: Ban

Katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa kumefanyika tukio maalum la maadhimisho ya miaka 20 tangu mkutano wa dunia kuhusu maendeleo ya jamii huko Copenhagen, Denmark ambapo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema umaskini bado ni jambo ambapo kizazi cha sasa kinapaswa kutokomezwa. Taarifa zaidi na Assumpta Massoi.

(Taarifa ya Assumpta)

Hotuba ya Ban pamoja na kutambua harakati mbali mbali kama vile mkutano wa wanawake Beijing na Malengo ya milenia katika kusongesha maazimio ya mkutano wa Copenhagen kama vile kutokomeza umaskini uliokithiri, amesema bado utu wa mtu unapaswa kuzingatia katika harakati za kiuchumi ikiwemo uhifadhi wa mazingira.

(Sauti ya Ban)

“Mara nyingi siku zilizopita, watunga sera wamejikita katika ukuaji wa uchumi, bila kutia maanani hofu ya kijamii au masuala ya mazingira. Lakini leo tuna ushahidi wa kuthibitisha kuwa ukuaji pekee hautoshi. Copenhagen ilibadili mtazamo kuwa ukuaji wa kiuchumi upimwe na athari zake kwa hali ya binadamu na si ukuaji pekee.”

Naye Juan Somavía, mshauri maalum wa Katibu Mkuu kuhusu ushirikiano wa kisera kwenye kanda akihutubia kwa njia ya video akatoa tathmini yake ya baadhi ya vikwazo..

(Sauti ya Somavía)

“Mchakato wa utandawazi ambao umekuwepo wakati malengo yote ya mikutano yametekelezwa, ulikuwa kinyume na maadili ya msingi ambayo yalikuwepo wakati mikutano ya miaka ya 90 ilifanyika.”