Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ujumbe wa UM waelekea Malawi kutathmini athari za mafuriko

Ujumbe wa UM waelekea Malawi kutathmini athari za mafuriko

Jopo la wataalamu wa Umoja wa Mataifa wa kutathmini kiwango cha majanga linatarajiwa nchini Malawi ili kusaidia harakati za kujikwamua baada ya mafuriko makubwa yaliyosababisha vifo vya watu 48 na wengine Laki Moja kupoteza makazi yao.

Taarifa hizo ni kwa mujibu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa inayohusika na usaidizi wa kibinadamu, OCHA ambapo tayari serikali ya Malawi imetangaza hali ya tahadhari kutokana na mafuriko hayo yaliyosababishwa na mvua zilizonyesha wiki chache zilizopita.

Ujumbe huo unaelekea Malawi huku serikali ya Malawi kwa kushirikiana na Umoja wa Mataifa na wadau wa kibinadamu ikiendelea kutoa misaada kwani mafuriko hayo yameharibu siyo tu miundombinu bali pia mazao na mifugo.

Ripoti zinasema Wizara ya Fedha ya Malawi imetenga zaidi ya dola Milioni Moja kusaidia harakati za kujikwamua kutoka zahma hiyo.