Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban amteua Meja Salihu mkuu wa UNMIL

Ban amteua Meja Salihu mkuu wa UNMIL

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amemteua Meja Jenerali Salihu Zaway Uba wa Nigeria kuwa Kamanda Mkuu wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Liberia, UNMIL.

Mteule huyo anachukua nafasi ya Muriuki Ngondi wa Kenya.

Meja Jenerali Uba ana uzoefu wa miaka 32 katika maswala ya kijeshi kitaifa na kimataifa. Pia amewahi kufanya kazi kama kamanda wa mafunzo, jeshi la Nigeria na afisa wa jeshi la nchi hiyo katika kituo cha ulinzi wa amani. kati ya mwaka 2013 hadi 2014.