Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hali ya chakula Sudan Kusini imeboreka lakini kuna wasiwasi:FAO

Hali ya chakula Sudan Kusini imeboreka lakini kuna wasiwasi:FAO

Kwa mujibu wa Shirika la Chakula na Kilimo, FAO hali ya chakula Sudan Kusini imeboreka, lakini bado kuna wasiwasi watu wengi hawana chakula cha kutosha.

Taifa hilo changa limekuwa likikabiliwa mapigano kati ya serikali na vikosi vya waasi tangu Desemba 2013 iliyopelekea karibu watu milioni mbili kukimbia makwao.

Evans Kenyi, ni mchambuzi wa usalama wa chakula wa FAO

“Mwezi Mei mwaka jana zaidi ya watu milioni 4.5 walikuwa katika hali ya dharura na mgogoro, lakini kwa wakati huu, tuna watu milioni 2.5 ambao wako katika hali ya dharura na mgogoro”