Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Lazima kushughulikia vichochezi vya uhamiaji haramu: IOM

Picha: IOM

Lazima kushughulikia vichochezi vya uhamiaji haramu: IOM

Ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya uhamiaji Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban ki Moon ametaka ulinzi wa haki za binadamu kwa kundi hilo ambalo ni zaidi ya milioni 200 kote duniani. Taarifa zadi na Amina Hassan.

(TAARIFA YA AMINA)

Katika ujumbe wake wa kuadhimisha siku hii Bwana Ban amesema wahamiaji wengi wanaishi na kufanya kazi katika mazingira magumu huku wakikumbana na unyanyasaji mbalimbali. Ametaka mipango ya maendeleo endelevu isiliache kundi hilo akisema kuwa lazima dunia ijali masilahi yake.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kimataifa  la Uhamiaji, IOM William Lacy Swing amesema lazima kushughulikia Vichochezi vya yanzo vya uhamiaji haramu hususan migogoro.

Akihojiwa na Daniel Dickinson wa radio ya Umoja wa Mataifa Bwana Swing amesema inasikitisha kuona maelfu ya wahamiaji wanafariki dunia wakijaribu kukimbilia nchi  mbalimbali kutafuta maisha bora.

Hata hivyo amesisitiza

(SAUTI LACY)

"Hili ni moja ya mambo muhimu tunayoweza kufanya, lazima tupunguze kutokea kwa majanga, lazima tufanye kila liwezekanalo kukomesha machafuko, lakini kwa bahati mbaya hakuna michakato ya  kisiasa yenye matumaini, hakuna mazungumzo yenye tija na tumaini la kukomesha punde machafuko."

Naye mhamiaji Laurence Kibatara aliyeko nchini Unigereza anazungumzia madhila wanayokumbana nayo wahamiaji.

(SAUTI LAURENCE)