Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la usalama lapitisha azimio la kuongeza muda wa kufikisha misaada Syria

Wafanyakazi wa UNSMIS wakishugulikia kazi ya tume ya kutafuta ukweli katika kijiji cha Mazraat al-Qubeir , Syria. Picha: UNSMIS / David Manyua

Baraza la usalama lapitisha azimio la kuongeza muda wa kufikisha misaada Syria

Baraza la usalama leo limepitisha kwa kauli moja azimio la kuongezwa kwa muda wa kufikisha misaada ya kibinadamu katika maeneo yanayokaliwa na waasi hadi ifikapo January mwaka 2016.

Azimio hilo linatoa mamlaka ya kutumia mipaka ya Uturuki, Iraq na Jordan bila ya idhini ya serikali ya Syria.

Kwa mujibu wa ripoti za Umoja wa Mataifa watu zaidi ya 190,000 wameuwawa wakiwamo watoto zaidi ya 10,000 ikiwa ni matokeo ya mgogoro huo wa Syria ulioibuka mwaka 2011.

Akizungumzia azimio hilo mwakilishi wa Syria katika Umoja wa Mataifa Bashar Ja’afari amesema

(SAUTI BASHAR)

"Azimio linashughulikia suala la kufikisha misaada ya kibinadamu kwa watu wa Syria. Serikali ya Syria

mara kwa mara imekuwa mshirika katika operesehni zinzolenga katika kugawa misaada ya kibinadamu kote nchini Syria."

Balozi Ja’afari alikuw akijibu tuhuma kuwa serikali ya Syrai imekuwa kikwazo katika ugawaji wa misaada . Amesema vikundi vya kigaidi mathlani ISIL ndivyo vinavyowajibika katika kuzuia misaada kuwafikia walengwa nchini humo.