Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la usalama lajadili hali nchini Libya

UN Photo/Loey Felipe
Picha:

Baraza la usalama lajadili hali nchini Libya

Baraza la usalama leo limekuwa na kikao kilichojadili hali nchini Libya ambapo baraza hilo limesikiliza taarifa ya kamati ya kufuatilia usalama nchini humo.

Kamati hiyo pamoja na mambo mengine imeeleza hatua za kuchukua ili kukomesha machafuko ikiwamo udhibiti wa uuzwaji wa silaha nchini humo.

Na kisha mwakilishi wa Libya katika Umoja wa Mataifa balozi Ibrahim Dabashi akasema..

(SAUTI BALOZI)

"Wanachotaka Walibya kutoka kwa baraza hili ni mambo mawili. Kwanza kuwezesha jeshi la Libya kupata vifaa ili kufanikisha ushindi dhidi ya ugaidi na uasi ili kurejesha dola halali. Pili ni kusimamia mpango wa ujenzi wa taasisi ambao utekelezaji wake utaanza pale jeshi litakaposhika hatamu mjni Tripoli."