Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Harakati za upatanishi nchini baada ya kesi za ICC

UN Photo/Loey Felipe
James Gondi, Wakenya kwa amani na maridhiano. Picha:

Harakati za upatanishi nchini baada ya kesi za ICC

Punde baada ya kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi wa urais nchini Kenya na Mwai Kibaki kuapishwa kuwa Rais terehe 30 Desemba mwaka 2007, ghasia ilitanda nchini humo.

Hali hiyo tete, ilipelekea kuuawa kwa karibu watu 1500 huku wengine zaidi ya nusu milioni wakifurushwa makwao. Ili kurejesha hali ya amani nchini, Muungano wa Afrika, ulimteua Katibu Mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa, Kofi Annan kuongoza juhudi za upatanishi ambazo zilizaa matunda ya amani huku baadhi ya kesi zikiwasilishwa kwenye mahakama ya kimataifa ya makosa ya jinai, ICC huko Hague.

Katika makao makuu ya Umoja wa mataifa kwa wiki mbili kumefanyika mkutano wa 13 wa mwaka wa nchi wanachama wa mkataba wa Roma ulioanzisha mahakama hiyo ambapo unakamilika Jumatano tarehe 17 Disemba ukiangazia masuala kadhaa.

Katika makala ifuatayo Abdullahi Boru aangazia hali ya upatanishi miongoni mwa jamii hasimu sawia na kesi za ICC.